IMG-20171102-WA0041
All Posts, Featured,

SHOW: Mahojiano ya Mboni Masimba na Omby Nyongole!.

Unavyo ishi vizuri na watu jua kabisa umejiwekea akiba ya baadae, Omby Nyongole ni school mate wa Mboni Masimba tangu Shule ya Msingi (P rimary) urafiki wao umedumu toka enzi hizo mpaka sasa bado wanaendelea. Akizungumza Mkurugenzi wa The Mboni Talk Show Mboni Masimba kuhusu urafiki wake na Omby  amefafanua  kama ifuatavyo.

“Omby aliondoka nchini Tanzania 2001  na kwenda kufanya makazi yake nchini Marekani, lakini kizuri tunachojivunia mimi na yeye hatukuacha kuwasiliana miaka yote hiyo tulikuwa tunawasiliana mara kwa mara. Nilifurahi sana kumuona Omby baada ya Miaka kadhaa kupita.. Omby anaishi Washington DC na yeye ndio aliwashawishi waandaaji wa Tanzania Day kunialika ili nikafanye coverage kwenye event, na yeye hakusita kutoka Dc kuja kuniona na kuni-support SHOGAREEEEE ahahah.

Kitu nilichompendea mate wangu “KISWAHILI CHAKE KIKO PALE PALE KIMENYOOKA NA SIO WALE WENGINE WAMEKAA MIAKA MIWILI NNJE YA TANZANIA LAKINI KISWAHILI KIMEPOTEA – Wanasema “KISWAHILI YANGU SIO MUZURI”ahahaha Pata kumsikiliza kidogo Mate wangu#Rafiki yangu #Ndugu yangu”

Leave Comment